Friday, July 29, 2016

18+KWA WANAUME WENYE TATIZO LA KUFIKA HARAKA WAKATI WA TENDO LA NDOA ,TUMIA MBINU HIZI ZITAKUSAIDIA.ACHANA NA MADAWA

Watu wengi wana tatizo hili usiwaone wamevaa masuruali hawasemi tu, kwa machache tu kwa ufahamu mchache nilio nao,Kwanza fanya mazoez ya kuzuia kukojoa...mimi binafsi niliwah kupiga nyeto kwa vipindi tofaut huko nyuma......ila nilikua napenda sana ile raha ya kutaka kumwaga niendelee kuisikia japo kwa dakika kadhaa,.........kumbe kule kujichelewesha kulinipa ex[perience nyingine!!nilijikuta baada ya muda fulani ninauwezo wa kukontroo nikojoe baada ya muda gani,,,nilipoingia rasmi kwenye uhusiano na laazizi wangu aliniona pamoj ana sifa nyingine zakipekee nilizo nazo kuwa mwanaume wake never seen....si kwamba najisifia ndugu ila nina uwezo kwa kukaa juuya kifua cha mwanamke hata kwa dakika 30...bila kupiz na hapo ni hadi aniambie plz beby come..try that na uniambie..pili jua Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki. Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza, isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio anakua yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA). Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote… ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio)… unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira, ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri. Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride) Concetration/ Umakini uliopitiliza… Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako (level of concentration). Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo… haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana….. Usiweke sana akili yako hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili na umahini wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga ‘PUSH-UPS walau 50’’ kila siku na ‘’SQUARTS’’ . haya ni mazoezi mepesi lakini ni BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli ''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya Pia Afya ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................ Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi

Thursday, July 28, 2016

UTAFITI: Kutazama TV kunaweza kusababisha kifo.

Utafiti huu umeripotiwa na BBC ambapo imeelezwa kuwa umefanywa na wanasayansi wa Japan ambapo umethibitisha kwamba kukaa kwa muda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa saa nyingi  kunahatarisha afya kwani kunahusishwa na maradhi yanayosababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.

Watafiti hao wamesema hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu husababisha vifo.

Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku. Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miezi 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.

Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, hatari ya kupata ugonjwa wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40.

Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa muda wa chini ya saa 3.

Aidha watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.

JE WAJUA WATANZANIA WENGI HUTAFUTA NINI KWENYE MTANDAO??

Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yameleta neema na mapinduzi makubwa Duniani. Tofauti na nchi zilizoendelea ambazo zimeingia kwenye ulimwengu wa mtandao muda murefu, Suala la mtandao linaonekana Jipya kwa watanzania walio wengi, na Wengi wao wanataman kuona kuna nini huko ndani? Ujio wa simu za kisasa (smartphones) umekuwa jibu na suluhisho la tatizo hilo.

JE WAJUA WATANZANIA HUTAFUTA NINI KWENYE MTANDAO?

Hivi ni Vitu Kumi Zaidi Wanavyovitafuta Watanzania (Kwa mujibu wa Kitafutio cha Google)

10.Biashara
Kutokana na kukua kwa kasi kwa uuzaji na ununuzi pepe (e-commerce) duniani, watanzania hawajaachwa nyuma sana japo ni idadi ndogo sana ya watanzania wanaoweza kufanya biashara mtandaoni. Wengi wa watanzania hutafuta na kuuza Magari, Simu za mkononi, pikipiki, nyumba na maeneo ya ardhi.

9.Vichekesho (comedy)
Utashangaa lakini hii ni moja ya vitu ya vitu vinavyotafutwa sana na Watanzania wengi kwenye mtandao, Wengi hutafuta video za kuchekesha, picha, na meseji za vichekesho. pia hupenda kuwajua wachekeshaji nk.

8.Elimu, mafunzo na afya
Kwa kiasi fulani kuna idadi ya watu wanaoingia kwenye mtandao kupata elimu inaongezeka, japo wahusika wengi hapa huwa wanafunzi hasa wa vyuoni ambao wengi hutumia google kupata majibu ya maswali waliyopewa na wakufunzi wao!

7.Michezo
Utakubaliana na mimi  kwamba watanzania wengi ni wapenda michezo (JAPO HAWAPENDI MAZOEZI YA VIUNGO) Wengi wa Watanzania huingia mtandaoni kupata habari za soka hasa za bara la ulaya.

6.Siasa
Uelewa wa Watanzania katika Siasa umekua ukiongezeka siku hadi siku na kumekuwa na idadi kubwa sana ya Watanzania wanaotafuta habari za siasa mfano; bunge, bajeti ya nchi, mahusiano ya nchi yetu na mataifa mengine, Vyama vya siasa nk.

5. Mahusiano & Kutafuta wapenzi
Kama ilivyo kwa nchi nyingi Duniani, Kumekuwa na idadi kubwa sana ya watu wanaotembelea mitandao ya kutafuta wapenzi, ushauri wa mapenzi, nk japo kuna unafuu kwetu (pengine ni kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupata intaneti) kulingananisha ni nchi zingine kama nigeria na kenya.

4. Kutafuta Video, Muziki , na Programu za computer/simu
Kuna idadi kubwa sana ya Watanzania Wanaotafuta vitu hivi, Cha ajabu na Kwamba Video nyingi zinazotafutwa ni zile zenye maudhui ya kikubwa (adult movies). Pia nyimbo Zinazoangaliwa zaidi youtube ni zile zinazoonesha watu wakicheza bila maadili.

3. Kusoma na Kutuma Barua pepe
Watanzania walio na uwezo wa kuingia mtandaoni, Wengi wao wana anuani za Barua pepe japo ukweli ni kwamba kati ya watanzania 10 wenye anuani za barua pepe, ni watanzania watatu (3) tu ndio wenye Uelewa juu ya barua pepe na kuzitumia. 7 waliobaki pengine walifungua anuani ya barua pepe kwa kushurutishwa au ili tu wajiunge na mtandao fulan wa kijamii hasa facebook.

2.Blog na Magazeti
Blog na Magazeti zinashika nafasi ya pili kati ya vitu vinavyosomwa zaidi na watanzania kwenye Mtandao. Watanzania wengi hupenda kujua habari muhimu kuhusu yanayoendelea nyumbani na kimataifa pia, michezo, burudan nk. Watanzania pia hupenda kuangalia watu fulani mashuhuri kupitia blogs mbalimbali.

1. Mitandao ya kijamii
Najua utakubaliana na mimi kwamba karibu kila mwenye uwezo wa kuingia mtandaoni basi ameshajiunga na moja kati ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, LinkedIn, Instagram, nk. Hii ndio inayoongoza kutembelewa na watanzania walio wengi zaidi kuliko kingine chochote.

MBINU TANO ZA KUANZA NA KUKUZA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO.

Leo katika kipengele hiki tutaona jinsi ya kukabiliana na changamoto hii. Lakini kabla hatujaona ni nini cha kufanya, hebu tusome maoni ya msomaji mwenzetu.
Nilikuwa nimeajiriwa na Wazungu fulani. Walipoondoka nilianza kigenge cha laki mbili sasa naendelea mdogo mdogo. Changamoto yangu ni kukuza na kupata duka la jumla. tatizo ni wapi nitapata mtaji usiozidi milioni kufikisha malengo yangu, nitumie njia gani maana kigenge changu pato lake halizidi 40 kwa siku, naomba ushauri nifanyeje. M.P
Kama tulivyosoma alichoandika msomaji mwenzetu hapo juu, ameanza biashara na mtaji kidogo na sasa changamoto yake ni kuikuza biashara hiyo zaidi. Hapa tutashirikishana baadhi ya mambo ya kufanya ili kuweza kukuza biashara hii na kufikia mafanikio makubwa.

1. Jipe muda, biashara haitaweza kukua haraka kama unavyofikiri

Uzuri wa kuanza biashara na mtaji kidogo ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini pia urahisi huu wa kuanza biashara kwa mtaji kidogo unafanya ukuaji wa biashara kuwa wa taratibu sana. Hivyo unapofanya biashara yoyote ambayo unaanza na mtaji kidogo ni muhimu ukajipa muda ili kuweza kukuza mtaji wako. Usiwe na tamaa ya kutaka kukuza biashara hii haraka, unaweza kuingia kwenye maamuzi ambayo yatakugharimu zaidi. Endelea kufanya biashara yako huku ukijifunza zaidi na kuangalia kila fursa ambayo unaweza kuitumia kukuza biashara yako.

2. Kuza mtaji wako taratibu

Kwa mtaji huo mdogo ambao umeanza nao biashara, endelea kuukuza kila siku. Usiendeshe biashara kwa kula kila kipato unachopata, badala yake tenga sehemu ya akiba irudi kwenye biashara yako. Fanya hivi kwa nidhamu ya hali ya juu sana na unahakikisha kila unapopata faida sehemu inarudi kwenye biashara yako. Pia endelea kuangalia kwa mazingira uliyonayo na kwa biashara unayofanya ni kwa jinsi gani unaweza kukuza mtaji wako zaidi. Kama utafikiria hili kila siku, hutakosa majibu ambayo yatakusaidia.

3. Punguza gharama za biashara na za maisha pia

Kuwa kwenye biashara haimaanishi kwamba ndio una uhuru wa kufanya chochote unachotaka na fedha za biashara hiyo, kwa sababu tu ni zako. Wewe sasa upo kwenye wakati mgumu wa kukuza biashara yako huku ukiwa huna njia nyingi za kufanya hivyo. Hebu kwa sasa punguza kabisa gharama zako za kibiashara na za maisha pia. Kama kitu sio muhimu sana basi usikigharamie. Punguza matumizi yote ambayo ni ya anasa tu na sio kwa ukuaji wa biashara. Katika kupunguza gharama zako za biashara na maisha, jijengee nidhamu nzuri sana ya fedha. Usitumie fedha kiholela tu, kuwa na mahesabu na sababu kwa nini umetumia fedha fulani, hasa kwa matumizi ambayo sio ya kawaida.

4. Angalia watu ambao unaweza kushirikiana nao

Baada ya kuiendesha biashara yako vizuri na ukaona inaenda kwa faida, unaweza kuangalia watu ambao unaweza kushirikiana nao kwenye biashara hiyo. Kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa na mtaji lakini hawana muda wa kufanya biashara. Lakini pia watu hawa wanataka mtu ambaye wanaweza kumwamini. Hivyo kama unaweza kuaminika angalia watu unaoweza kushirikiana nao kibiashara. Andaa mpango mzuri ambao utamshawishi mtu ni jinsi gani yeye atafaidika kama atawekeza kiasi kidogo kwenye biashara yako. Ikiwa unaendesha biashara yako kitaalamu itakuwa rahisi zaidi kushawishi watu kushirikiana na wewe.

5. Rasimisha biashara yako ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mkopo

Hata kama biashara yako ni ndogo kiasi gani, irasimishe. Iendeshe kisheria kwa kuwa na namba ya mlipa kodi na hata leseni pia. Hivi vitakuwezesha wewe kutambulika na taasisi za kifedha pale utakapohitaji msaada zaidi wa kifedha. Mkopo kwenye taasisi za kifedha ni chanzo muhimu ila usikimbilie kama bado hujaweza kuiendesha biashara yako kwa faida. Hakikisha umeiweka biashara yako vizuri kwanza na inajiendesha kwa faida ili unapochukua mkopo unajua unauweka wapi na kuendelea kupata faida zaidi. Kuikuza biashara pale ambapo umeanza na mtaji kidogo ni kitu ambacho kinawezekana. Ila unahitaji kujitoa na kujenga nidhamu kubwa. Unahitaji kufanya kazi zaidi ya wafanyabiashara wengine, unahitaji kuwa mbunifu wa hali ya juu na pia unahitaji kujijengea uaminifu. Ukishajua wewe biashara yako ni ndogo na inahitaji kukua, basi hakikisha kila mara unaumiza akili yako ifikirie njia zaidi za kuikuza. Na kama utaweza kufanya hivi basi utaziona fursa nyingi zilizokuzunguka za kuikuza biashara yako.

WATAFITI WADAI MENDE WA AINA HII WANA MAZIWA YENYE PROTEIN KULIKO NG'OMBE.

Uchunguzi wa wanasayansi umebaini maziwa ya mende yana virutubisho ya protini mara nne zaidi ya ng’ombe. Taarifa ya timu hiyo ya kimataifa ya wanasayansi hao ya ‘Institute of Stem Cell Biology and Regenerative Medicine’ ilisema maziwa hayo yanaweza kuwa muhimu kuwalisha watu wanaoongezeka duniani siku za usoni.

Sehemu ya taarifa hiyo ambayo imenukuliwa na mashirika mbalimbali duniani imesema……>>>’Ingawa mende wengi hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera punctute, wameonekana kutoa utomvu unaoonekana kama maziwa yenye protini yanayotumika kuwalisha watoto’

Taarifa hiyo imesema wadudu nao hutoa maziwa lakini kilichowashangaza zaidi watafiti ni yana nguvu mara tatu zaidi yanayopatikana kwenye maziwa ya kifaru.

THE 8 MONKEYS .

The 8 Monkeys (This is reportedly based on an actual experiment conducted.) Put eight monkeys in a room. In the middle of the room is a ...