Baada ya uchunguzi wa kisayansi kubaini kwamba maziwa ya mende yana protini mara nne zaidi ya maziwa ya ng’ombe na kifaru, imebainika kwamba maziwa ya mende pia hutumika kwa matibabu mbalimbali ya binadamu.
Miongoni mwa matibabu hayo ni pamoja na kutengeneza miguu bandia ya kutumiwa na binadamu, mtafiti mkuu katika mradi uliofanyika katika Chuo Kikuu cha A&M cha Texas Hong Liangnchini Marekani amesema…….>>> ‘Nilipoona hii kwa mara ya kwanza nilishangaa’
Alisema wanasayansi kwa miaka mingi wamekua wakishangazwa na uwezo wa mende wa kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika, wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupambana na sumu.
Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria wanaoathiri zaidi watu kwa mfano E.Coli na MRSA ambao hawauliwi kwa dawa yoyote.
Hii siyo mara ya kwanza mende kuhusika kwenye matibabu, Mwandishi Lafcdio Hearn Karne ya 19, alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokua wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kuwekwa kwa mende aliandia kuwa …….>>>’Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani na tiba hiyo’
Pia alisema China kuna mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende. Hutumiwa kutumiwa vidonda vya moto pia humezwa kutibu vidonda tumbo. Kuna aina 4500 ya mende na aina nne pekee ambao huwa waaribifu.