Saturday, July 30, 2016

KWA WANAUME SOMA HII YA HUYU MTAFITI, UTAJIFUNZA KITU.

_*Na, Mtafiti.*_
     _Mwanaume_
           24/07/2016.

MWANAUME  _unatakiwa kujitambua na kujiheshimu  bila kusahau kuutunza ujana wako kwa maneno  yenye hekima na busara ,kama wewe ni kijana na haujaoa na una miaka  25 kwenda juu basi jua wewe ni baba pasipo mtoto jiandae  kuwa baba bora na mume bora kwa matendo na mawazo bila kusahau kuitunza haiba yako ya kiume kwa mavazi safi na bora._

MWANAUME _anayejiheshimu huwa hanyoi kiduku hata siku moja ,kijana bora mwenye kujitambua huwa sio mtumwa wa pombe hata siku moja,kuwa na idadi kubwa ya wanawake sio ujanja bali ni utumwa wa fikra  sababu unatakiwa uitawale pombe na wanawake .sasa ni wakati sahihi wa kuacha ujinga a kujiaanda kuwa mume bora na baba bora._

MWANAUME_ _anayejitambua havai nguo za kumbana mapaja ,havai mlegezo wala   havai nguo za kumbana makalio, mtoto wa kiume  ,jaribu kuwa Muungwana sababu  neno mwanaume limebeba ubora wa utashi wa fikra na tabia ._

_Wanawake wanapenda wanaume wenye upeo mkubwa na  wanao jiamini sababu mwanaume  ni kiogozi na kichwa katika familia sasa unawezaje kuwa kichwa cha familia na kiduku  huku ukiwa na mlegezo ?_

_Wewe ambaye upo  chuo ujanja si kupiga selfie na wanawake   au kushinda kwenye Instagram part kila weekend ,badilika sasa na acha ujinga tumia chuo kama kiwanda cha maarifa na  sio sehemu ya fashion show na mashindano ya kununua smart phone ,kuwa mwanaume bora ili ukikutana na wanaume  wenzio uzungumze kama mwanachuo aliyekomaa nasio kulamba lamba midomo_

_Ongeza idadi ya kusoma vitabu na sio kuwa  mashindano ya kuwa  na idadi  nyingi ya likes za picture za swagger na wingi wa majina yasio na tija ,kumbuka Kendrick Lamar  alitengeneza Brand ya jina lake na wewe tengeneza Brand name yako na sio kuiga ujinga usio na tija.You cannot change yesterday, but you can change today and tomorrow. #Modern Gentleman._

_By Mtafiti._.

THE 8 MONKEYS .

The 8 Monkeys (This is reportedly based on an actual experiment conducted.) Put eight monkeys in a room. In the middle of the room is a ...