Sunday, May 14, 2017

THE POWER OF THINGKING (NGUVU YA KUFIKIRI CHANYA)

POWER OF THINGKING
(NGUVU YA KUFIKIRI)
Mwandishi:(procurement officer) Elisante jumanne Ngoma.
Phone:0672205433
Huwa watu walio wengi wanafikiri kidogo sana.kufikiri kidogo kule kufanya kitu ambacho hakiwezi kuleta badiliko chanya kwenye jamii nzima au Kwa watu wengi.
Wasomi walio wengi huwa hawafikirii mbali sana japo kuwa wamejifunza mambo mengi sana,Na hii nikutokana Na kujiskia au kujiona wana elimu kubwa sana (Proffesa,PhD,master,bachelor au diploma)ambazo Kwa dunia ya sasa hazitoshi kuwafikisha wanapotaka,cha ajabu wanabaki wakishangaa kwamba mbona flani hajasoma Leo hii ni tajiri namba moja tanzania (bakresa).
Nawashangaa sana wanaojiita wasomi hali ya kuwa kila kitu wanachokifanya wana copy Naku peste hakuna anae kaaa Na kufikiri tofauti alafu tunajiita wasomi!!.
Public speaker mmoja anaitwa Mh : Hassan Nassor Ngoma alishawahi kuniambia kuwa " degree yako Kwa dunia ya sas hivi ni bure kama huwezi kufikiri tofauti".
Kuna nguvu kubwa katika uwezo wa kufikiri Na kufikiri hakuhitaji elimu wala nini,ni kuamua tu Na mwisho kuthubutu ulichokifikiri.
Huwa nilikaa Na kujaribu kujiuliza kuwa kuna dhambi gani katika kufikiri vitu vikubwa? Lakini je wote walio fikiri vitu vikubwa Na wakafanikiwa nao si binadamu kama sisi? Akina bill gate mgunduzi wa soft ware au marck zucrkbugy mgunduzi wa facebook unayoitumia Leo mbona nao ni binadamu kama Mimi? Tena wanakula kama mimi istoshe wana kufa kama Mimi, tatizo ni nin?
Nikagundua kuwa tatizo ni kitu kinachoitwa (falas) huu ni ukuta au mitazamo hasi ya watu wanao tuzunguka,Na hii inaweza ikaanzia ndani ya familia ,marafiki,marafiki ndugu pamoja Na jamaa wa karibu yako.
Mfano mzuri tu tokea ukiwa shule ya msingi au ukiwa mdogo kabisa labda ulishawahi kumwambia baba Yako au mama yako kuwa " lazima nitamiliki kiwanda cha kutengenezea ndege zinazotumia jua " Nina uhakika kuwa mzazi wako alicheka kisha akakuambia mwanangu umelogwa wew yani unafikir vitu vikubwa hvyo nawakati hata baiskeli wala nini huna.
Hvyo basi hizo (falas)zinaanzia tokea utotoni kabisa ambazo ndio zinamkosesha MTU ile nguvu ya kufikiri vitu vikubwa sana.
Ila jaribu pia kujiuliza mbona mark zurckburgy ameweza Na alikuwa Na wazaz? Hivyo Basi amua sas kufikiri vitu vikubwa kwani inawezekana hata utukanwe vip,uchekwe vipi,ukatishwe tamaa vipi wew fikiri ukishafikiri thubutu kukifanya hicho ulichofikiri.
Nina uhakika utafanikiwa sana.
Mwandishi mmoja wa vitabu (erick Shigongo ) alishawahi Kuniambia kwamba " Huwezi kufanikiwa bila kudharauliwa".Na Mimi pia nakuongezea kuwa " ukiona umekatishwa tamaa sana kuhusu jambo flani Basi jua hilo jambo ukilifanya ndio utafanikiwa sana".
Kwahyo utakapo kuwa unafikiri vitu vikubwa Basi wengi watakukejeli Na kukukatisha tamaa kuwa haiwezekani kutokea.
Ila nikuhakikishie kuwa wew fikiri alafu thubutu kufanya bila kujali kudharauliwa utaona matokeo Makubwa sana kwenye maisha yako.
Hivyo basi ukiwa mtoto,binti,kijana au Mzee una uwezo wa kufikiri vitu vikubwa Na vikaleta mabadiliko chanya kwenye jamii yako Na kukufanya ufanikiwe Kwa kiwango kikubwa kuliko ulivyotarajia.
Hata kama hujaenda shule kabisa,wewe fikiri tu Kuna nguvu kubwa katika kufikiri.
Nitakuwa Na mada mbali mbali kila siku hivyo Basi usichoke kufatilia kwenye account yangu ya fb au page yangu ya fb ELLYNEY COMPANY,pia unaruhusiwa Ku share sehem mbali mbali ili Ujumbe ufike Kwa wengi.
Kwa ushauri wa bure Na Msaada wa kufikia malengo yako wasiliana nami 0672205433
USIOGOPE KUFIKIRI

THE 8 MONKEYS .

The 8 Monkeys (This is reportedly based on an actual experiment conducted.) Put eight monkeys in a room. In the middle of the room is a ...