Ushawahi kuona mtu anajenga jela yake mwenyewe na kuiremba kisha kuchagua magereza wa kumlinda, mtu alieogopwa na wauza madawa wenzake na kuwaweka majaji, polisi na wanasiasa mfukoni kwa pesa ama vitisho. Moja ya watu wakatili aliemuondoa yoyote aliekuwa kikwazo katika njia yake akiwa na sera ya aidha ukubali rushwa au risasi za Pablo. Anaitwa Pablo Escobar a.k.a El Doctor, El Patrón,Don Pablo,El Señor, El Magico. Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR return ya $200. Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye njaa kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo kwa haraka haraka ni $b1, Panya walizokuwa wanakula.
*Marekani* na Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe. Akakubali but Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama 5star hôtel. Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao vya thamani. Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana uwezo wa kutoka na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa anawahonga vizuri sana. Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka kurudi kitaa, akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na walinzi wake wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto akaugua ghafla na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo alochofanya? Aliwasha moto wa kutoa baridi la ugonjwa wa kwa mwanae kwa kutumia noti zaidi ya 2million dollars, ziliwasha moto mtoto aote moto kupata joto, na kupika kwa note za $2,000,000, za kibongo ni b3 na m240. Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 = tsh 4,050,000 za kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka alikuwa ananunua rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela yake (hata BOT hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi kutokea kwa mtu wala taasisi) Alinunua ndege kwa ajili ya kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege ilikuwa inabeba $10m. Mwaka 1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7 duniani, anakadiriwa kuwa na utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu wanasema alikuwa anazidi hata hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio chini ya $60m, coz kwa mwezi alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA. Na ubabe wake wote, Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka Jela, serikali na jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo, akawa-offer serikali iachane nae na atailipia serikali deni ililokuwa inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni 18 za kibongo, ili serikali imalize deni inalodaiwa, lakini serikali ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa wamarekani na kumuua December 2/1993. Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni hiyo ya $10b ya Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd = trilioni 18.